Responsive image
Responsive image
Posted : February 08, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
mahakama ya ICC
Responsive image

Mahakama ya kimataifa ya makosa ya Jinai (ICC) imeifahamisha serikali ya Phillipines kwamba itaanza uchunguzi wa awali kuhusiana na mauaji holela yaliyofanyika nchini humo, chini ya kampeni dhidi ya dawa za kulevya.

Msemaji wa Rais amesema Rais Rodrigo Duterte wa Phillipines amekaribisha uchunguzi huo wa awali kuhusu madai hayo.

Rais Duterte amesema yuko tayari kufikishwa mahakamani iwapo kesi hiyo itaendelea na kuongeza kwamba iwapo kutakuwa na haja atajitetea binafsi ICC.

Mwanasheria mmoja nchini Phillipines amewasilisha mashitaka akimshutumu Rais Duterte na maafisa wengine waandamizi 11 kwa kufanya mauaji ya watu wengi mnamo Aprili mwaka jana wanaotuhumiwa kwa uhalifu na wauzaji wa dawa za kulenywa tangu rais huyo alipoingia madarakani Juni 30, 2016.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment