Responsive image
Responsive image
Posted : February 07, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
John Bocco wa timu ya Simba akijaribu 'kumtoka' Yakubu Mohamed wa Azam
Responsive image

Timu ya Simba imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara baada ya kuinyuka AZAM bao moja kwa sifuri.

Simba imejipatia bao pekee la mchezo huo kupitia kwa nyota wake Emmanuel Okwi aliyefunga katika dakika ya 37 baada ya kuunganisha krosi iliyochongwa vyema na beki Asante Kwasi.

Baada ya mchezo huo, nahodha wa Simba John Bocco amesema mchezo huo ulikuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wao huku nahodha wa Azam kwenye mchezo huo Agrey Morris akisema kutokutumia vyema nafasi walizopata ndio kilichowagharimu kwenye mtanange huo.

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha alama 41 na kuendelea kukalia usukani wa ligi hiyo huku Azam ikitua rasmi katika nafasi ya tatu ikiwa na alama 33 na Yanga kubakia kwenye nafasi ya pili baada ya jana kuibugiza Njombe Mji mabao manne kwa nunge na kufikisha alama 34.

ASHER THOMAS

07 FEBRUARI 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment