Responsive image
Responsive image
Posted : February 07, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres
Responsive image

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameitaka serikali ya Maldives kuondoa hali ya hatari na kuhakikisha usalama wa raia wake wakiwemo watumishi wa idara ya mahakama ya juu ambako jeshi limevamia.

Wito huo umekuja baada ya rais wa Maldives Abdullah Yameen, kutangaza hali ya hatari na vikosi vyake vya usalama kuivamia mahakama ya juu na kumshikilia Jaji Mkuu wa mahakama hiyo pamoja na jaji mwingine. 

 Taarifa iliyotolewa na msemaji wake Stephane Dujarric imesema kuwa Guterres anaisihi serikali ya Maldives kuheshimu katiba na utawala wa sheria hivyo kuondoa amri ya hali ya hatari haraka iwezekanavyo na kuchukua hatua zote kuhakikisha usalama wa watu nchini humo.

Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu hali inayojitokeza nchini Maldives, Tangazo la hali ya hatari na hatua ya vikosi vya usalama kuingia katika eneo la mahakama.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment