Responsive image
Responsive image
Posted : February 01, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Mbunge Tom Kajwang aliyekamatwa kwa tuhuma za kuhusika na uapisho wa Raila Odinga
Responsive image

Polisi nchini Kenya wamemkamata mbunge mmoja ambaye anadaiwa kuhusika katika hafla ya kumuapisha kiongozi wa upinzani nchini humo, Raila Odinga, kuwa 'rais wa wananchi'.

Kukamatwa kwa mbunge huyo wa upinzani kumekuja wakati ambapo serikali imevifunga vituo vitatu vya runinga na vya redio.

Mbunge huyo Tom Kajwang alikamatwa na kundi la maafisa wa polisi waliokuwa wamevalia nguo za kiraia Mjini Nairobi.

Vituo kadhaa vya runinga nchini Kenya vimefungiwa baada ya mamlaka ya mawasiliano kuzima mitambo yao kwa kujaribu kurusha moja kwa moja mkutano huo wa upinzani.

Waziri wa Usalama nchini Kenya Dokta Fred Matiangi amesema kuwa runinga hizo zitaendelea kufungwa hadi uchunguzi utakapokamilika kuhusu kuhusika kwao na kundi la upinzani dhidi ya serikali la NRM linalohusishwa na Muungano wa Upinzani NASA.

Chanzo BBC

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment