Responsive image
Responsive image
Posted : January 31, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Rais wa Marekani Donald Trump
Responsive image

Rais Donald Trump wa Marekani amewataka wananchi wa nchi yake kuungana na kuendelea kuimarisha uchumi wa taifa hilo unaoendelea kukua vizuri.

Akilihutubia bunge la Congress Trump amesema yuko tayari kufanya kazi na wabunge wa chama cha Democrat kuweka kando mgawanyiko mkali wa kisiasa baina ya vyama hivyo.

Amesema kwa pamoja wananchi wa Marekani wanaweza kushirikiana kukuza uchumi wa nchi hiyo ambao umeendelea kukua kwa kasi na kuongeza ajira.

Trump amesema chini ya uongozi wake taifa hilo limeendelea kufanya vizuri katika nyanja mbalimbali hivyo ni vema wananchi wakaungana na kuunda familia moja kubwa ya watu wa Marekani.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment