Responsive image
Responsive image
Posted : January 27, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Moto mkubwa uliowaka katika hospitali Korea Kusini
Responsive image

Zaidi ya watu 30 wamekufa na wengine 70 kujeruhiwa baada ya hospitali moja kuwaka moto Nchini Korea Kusini. Habari kutoka nchini humo zimesema kuwa zaidi ya wagonjwa 100 walikuwa ndani ya hospitali wakati moto ulipoanza kuwaka.

Inasemekana moto huo ulianzia katika chumba cha dharura cha Hospitali hiyo iliyopo kusini mashariki mwa nchi hiyo. Moto huo ulianza kuwaka katika chumba hicho cha dharura kilichopo katika ghorofa ya kwanza na kwisha kusambaa kwenye ghorofa ya pili.

Taarifa zimesema kuwa idadi kubwa ya wagonjwa waliokuwepo katika hospitali hiyo ni wazee.

Kufuatia ajali hiyo Rais wa Korea Kusini Moon Jae In ameitisha kikao cha dharura na baadhi ya viongozi wa serikali na kuiagiza serikali kuchukua hatua zote ili kusaidia walionusurika kwenye ajali hiyo.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment