Responsive image
Responsive image
Posted : January 25, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Mwigulu Nchemba
Responsive image

Serikali imetangaza kusimamisha utoaji wa hati za kusafiria za jumla kwa makundi mpaka utaratibu wa kuendelea kufanya hivyo utakapotangazwa.


Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es salaam, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hatua hiyo imekuja baada ya kupokea taarifa kuhusu vijana wanaosafirishwa kutoka Tanzania kwenda nchi za nje kwa kisingizo cha kufanya kazi llakini badala yake wamejikuta wakiangukia kwenye mateso na manyanyaso.

Katika hautua nyingine Dkt Mwigulu amezitaka taasisi zote zilizopewa vibali vya uwakala wa kutoa hati za kusafiria hapa nchini kuripoti ofisi za uhamaji kwa ajili ya uhakiki.

Waziri huyo pia amesema serikali itaendelea kushirikiana na nchi ambazo kuna watanzania wanaotumikishwa ili kukomesha vitendo hivyo.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment