Responsive image
Responsive image
Posted : January 25, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Zimbabwe anayemaliza muda wake nchini, Edzai Chimonyo
Responsive image

Rais Dkt. John Magufuli ameagana na Balozi wa Zimbabwe hapa nchini anayemaliza muda wake Edzai Chimonyo na kumuuomba

amfikishie salamu za pongezi Rais Emmerson Mnangagwa huku akimkaribisha aje nchini kutembea.

Taarifa ya Ikulu imemnukuu Rais Magufuli akisema "naomba umwambie Rais Mnangagwa kuwa namkaribisha atembelee Tanzania na namtakia heri katika majukumu yake, natarajia ataendeleza uhusiano na ushirikiano wetu ili tuweze kujiiimarisha zaidi kiuchumi kwa manufaa ya nchi hizi mbili".

Rais Magufuli pia amempongeza Balozi Chimonyo kwa uwakilishi mzuri alioufanya kwa miaka 10 aliyoiwakilisha Zimbabwe hapa nchini.

Chimonyo naye ameshukuru kwa ushirikiano mkubwa alioupata katika kipindi chake cha Ubalozi hapa nchini na amempongeza Rais Magufuli kwa namna anavyoiongoza nchi, huku akitaja baadhi ya mambo yanayofanywa kwa mafanikio makubwa kuwa ni mapambano dhidi ya rushwa na miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu. 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment