Responsive image
Responsive image
Posted : January 25, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako
Responsive image

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya ufundi, Profesa Joyce Ndalichako  amesema watu waache kupotosha kuhusu Sera ya elimu bure kwa kuwakataza wananchi kuchangia maendeleo ya elimu.

Profesa Ndalichako amesema kwa mujibu wa waraka wa elimu namba Tano mwaka wa 2015 na namba Tatu wa mwaka 2016 wazazi na kamati za shule zinaweza kujiwekea utaratibu kwa  wanaotaka kuchangia vitu mbalimbali ya shule ikiwemo chakula.

Profesa Ndalichako amesema serikali imekataza walimu kujikita kukusanya michango ya hiyari kutoka kwa wazazi inayochangwa kwa sababu mbalimbali.

Ndalichako yupo mkoani Njombe kukagua miradi ya elimu.

TATU  ABDALAH

JANUARI 25, 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment