Responsive image
Responsive image
Posted : January 25, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa kitengo cha ukuzaji biashara na masoko wa benki ya MCB Valence Luteganya (wa tatu kushoto) akiongea na waandishi wa habari katika uzinduzi wa huduma mpya ya benki hiyo ya Mikopo ya dharula.
Responsive image

Benki ya Biashara ya Mwalimu (MCB) imeanzisha huduma ya mikopo ya dharura ambayo rejesho lake hukatwa kwenye mshahara wa mteja (Salary advance) kwa lengo la kumwezesha mteja kuyakabili mahitaji muhimu yanayojitokeza wakati wowote.

Mkuu wa kitengo cha ukuzaji biashara na masoko wa benki hiyo Valence Luteganya amesema huduma ya 'Salary Advance' inawahusu wateja wafanyakazi wanaopitisha mishahara yao katika benki ya mwalimu ambao wataweza kupata mkopo wa hadi asilimia 50 ya mishahara yao.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment