Responsive image
Responsive image
Posted : January 25, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Mwanasheria wa Ofisi ya Taifa ya takwimu –NBS, Oscar Mangula,
Responsive image

Ofisi ya Taifa ya Takwimu imemfikisha mahakamani Mkusanya Takwimu wa Kijiji cha Nghulugano Wilaya Bahi Mkoani Dodoma, John Hima kwa tuhuma za kutokuwepo katika eneo lake la kazi na kushindwa kuteleza majukumu yake.

 

Akisoma mashtaka hayo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bahi, Msuniva Mwajombe, amesema mshtakiwa anatuhumiwa kutenda kosa hilo akiwa mdadisi wa mradi wa utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi nchini mwaka 2017/18.

 

Naye Mwanasheria wa Ofisi ya Taifa ya takwimu –NBS, Oscar Mangula, amesema suala kufikishwa mahakamani itakuwa fundisho kwa wengine ambao wanakwenda kinyume na viapo vyao vya kazi.

 

Mshitakiwa amekana kosa hilo na kurudishwa rumande hadi Tarehe SABA mwezi ujao baada ya kukosa wadhamini wawili wa kuaminika.

 

 

SHABAN KWAKA

JANUARI 25, 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment