Responsive image
Responsive image
Posted : January 24, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Responsive image

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameweka bayana mapenzi yake dhidi ya Rais wa Marekani Donald Trump kwa kusema anampenda Rais huyo kwa vile anazungumza hisia zake bila kuficha.

Rais Museveni ametoa kauli hiyo wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) jijini Kampala, Uganda ambapo amesema Marekani imepata rais bora na kwamba waafrika ni wadhaifu.na wanahitaji kutatua matatizo yao wenyewe

Kauli ya Rais Museveni inaonekana kupinga majibu ya viongozi wengi wa Afrika ambao walilaani matamshi ya hivi karibuni ya Rais Trump kuyaita mataifa ya Afrika kuwa ni ni machafu.

Utetezi wa Rais Museveni kwa Trump umekuja saa chache baada ya balozi wa Marekani nchini Uganda kumkosoa Rais Donald Trump.

Chanzo BBC

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment