Responsive image
Responsive image
Posted : January 23, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma
Responsive image

Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma amesema viongozi wa serikali watakaoingilia na kuvunja amri za mahakama watachukuliwa hatua za kisheria.

Jaji Juma ameyasema hayo jijini Dar es salaam katika mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu wiki ya sheria inayotarajiwa kuanza tarehe 27 ya mwezi huu na kusisitiza kuwa mahakama pekee ndiyo yenye mamlaka ya kutoa haki.

Maadhimisho ya wiki ya sheria yanatarajiwa kuanza Jumamosi wiki hii ambapo mahakama na wadau wa sheria watakuwa wakitoa elimu na msaada wa kisheria katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini kwa muda wa siku tano. 

Jaji Mkuu amesema hatavumilia kuona mtu yeyote anaingilia na kuvunja amri za mahakama.

Kwa upande wake Jaji Kiongozi Ferdinand Wambali amesema matumizi ya Tehama yataharakisha usuluhishi kwenye mahakama.

Maonyesho ya sheria yatatanguliwa na matembezi maalum ya kuadhimisha wiki ya sheria yanayotarajiwa kuongozwa na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete na mgeni rasmi katika kilele cha wiki ya sheria Februari Mosi mwaka huu anatarajiwa kuwa Rais Dkt John Magufuli.

LEVINA KATEULE

23 JANUARI 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment