Responsive image
Responsive image
Posted : January 23, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Juma Nyosso (aliyevaa tisheti ya kijani) akipelekwa rumande na polisi
Responsive image

Jeshi la polisi mkoani Kagera linamshikilia mlinzi wa kati wa timu ya Kagera Sugar Juma Nyosso kwa tuhuma za kumpiga shabiki wa timu ya Simba, Shaban Hussein mkazi wa Kemondo mkoani Kagera

Kamanda wa polisi Mkoani Kagera Augustino Ollomi amesema Nyosso anadaiwa kumpiga shabiki huyo baada ya kumpulizia vuvuzela usoni na kuongeza kuwa Nyosso atabaki Rumande mpaka uchunguzi utakapokamilika ili afikishwe mahamakani.  

Tukio hilo liliokea mara baada ya mchezo kati ya timu yake ya Kagera Sugar na Simba kumalizika ambapo Kagera Sugar walipoteza mchezo huo kwa bao mbili kwa bila.

Juma Nyoso ambae aliwahi kuichezea Simba kwa mafaniko siku za nyuma amerejea dimbani msimu baada ya kutumikia kifungo cha miaka miwili kutokucheza soka,  baada ya kumdhalilisha mshambuliaji wa Simba, John Bocco ambaye wakati huo alikuwa akiichezea Azam FC na Nyoso alikuwa akiichezea Mbeya City. 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment