Responsive image
Responsive image
Posted : January 23, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Kaimu Meneja Uhusiano wa DAWASCO Everlasting Lyaro
Responsive image

Shirika la maji safi na majitaka mikoa ya Dar  Es Salaam na Pwani (DAWASCO), limewataka wananchi kutoa taarifa za upotevu wa maji unaotokea mitaani ili kuokoa fedha inayopotea kutokana na upotevu huo.

Akizungumza jijini ar es salaam kaimu meneja uhusiano wa shirika hilo  Everlasting  Lyaro amesema maji yanayopotea ni mengi kwa mujibu wa viwango vya kimataifa na shirika hilo linafanyia kazi taarifa zote zinazofikishwa ili kuzuia upotevu huo.

Kuhusu majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea eneo la Buguruni Mnyamani, Lyaro amesema shirika linawahudumia majeruhi wawili wanaopatiwa matibabu na watoto watatu waliojeruhiwa katika tukio hilo watapatiwa vifaa vya elimu.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment