Responsive image
Responsive image
Posted : January 22, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
George Weah akila kiapo cha urais wa Liberia
Responsive image

George Weah ameapishwa mnamo saa sita kamili mchana leo Januari 22, 2018 katika uwanja wenye uwezo wa kubeba watu 35,000 wa Samuel Kanyon Doe, ulioko katika jiji maarufu la Liberia la Monrovia. Uapisho huo ulihudhuriwa na marais wasiopungua wanane wa  bara la Afrika ambapo Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, aliwakilishwa na Makamu  wake Yemi Osinbajo.

Uapisho huo George Weah umewaweka wa-Liberia katika furaha kubwa ambapo kwa mara ya mwisho mabadiliko ya uongozi yaliyotawaliwa na amani katika nchi hiyo kati ya marais wawili waliochaguliwa kidemokrasia yalitokea mwaka 1944 wakati Rais Edwin Barclay alipokabidhi madaraka kwa William Tubman.

Weah aliingia kwenye siasa baada ya kustaafu mchezo wa soka mwaka 2002 na alianza kugombea urais mwaka 2005 ambapo alizidiwa na Rais Ellen Johnson Sirleaf.

Wa-liberia wengi wanamuona Weah mwenye umri wa miaka 51 kama shujaa kutokana na historia yake iliyomtoa kwenye umaskni 'wa kutupwa' nchini Liberia hadi kumpeleka katika umaarufu mkubwa katika soka duniani.

Rais huyo mpya ameahidi kutokomeza rushwa na kuboresha uchumi wa nchi hiyo.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment