Responsive image
Responsive image
Posted : January 19, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Mke na mume wanaodaiwa kuwafungia ndani watoto na kuwatesa
Responsive image

Wapenzi wawili nchini marekani wanaotuhumiwa kuwafungia ndani watoto na ndugu zao 13 wamesomewa zaidi ya mashitaka 12 yanayoweza kuwapeleka jela kila mmoja miaka 94 au kifungo cha maisha.

Hakimu wa mahakama ya wilaya Riverside nchini Marekani Mike Hestrin amesema kesi ya wapenzi hao imegusa watu wengi ambapo imedauwa kuwa watoto hao walikuwa kwenye mateso makali ya kufungwa na minyororo na kukosa chakula kwa muda mrefu.

David Allen Turpin mwenye umri wa miaka 57, na mkewe Louise Anna Turpin (49) mwanzoni mwa wiki hii walikamatwa na polisi mjini Calfonia mara baada ya kupatikana kwa taarifa za kuwateka watoto hao.

Washitakiwa hao wamekana mashitaka na kesi yao kuahirishwa hadi Februari 23 mwaka huu itakapotajwa.

 

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment