Responsive image
Responsive image
Posted : January 17, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Baadhi ya askari wa jeshi la Nigeria
Responsive image

Jeshi la Nigeria limesema limewaachia huru watu 244 waliokuwa wakishukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Bokoharam.

Jeshi hilo limesema kuwa limewaachia watu hao ambao wamejuta kujihusisha kwenye kundi hilo na wamedai kubadilika tabia na wako tayari kurudi katika jamii.

Jeshi limewaachia huru watu hao ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya siku ya majeshi ya Nigeria.

Wachambuzi wanasema hatua hiyo inaweza kuhatarisha usalama wa raia wa nchi hiyo kwa kuwa huenda watu hao wakaendelea kujihusisha na kundi hilo.

Miongoni mwa walioachiwa huru ni wanawake na watoto ambao wamekabidhiwa kwa gavana wa jimbo la Borno eneo ambalo limeathiriwa na mashambulio ya kundi hilo.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment