Responsive image
Responsive image
Posted : January 13, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
Responsive image

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema mazungumzo kuhusu hatima ya kampuni ya Ubia kati ya  Shirika la Utangazaji Tanzania TBC na na Kampuni ya Star Times Group ya China yamemalizika hii leo na pande zote kuridhika na mapendekezo yaliyopendekezwa na serikali.

Akizungumza  na TBC Jijini Dar es salaam Dkt.Mwakyembe  amesema mkutano wa leo umefikia muafaka mzuri wa kupatikana kwa faida  baina  ya pande zote mbili na kwamba wataalamu wanaandika maazimio yaliyofikiwa ili umma uweze kufahamishwa .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kampuni ya Star Times Group Xinxing Pang amesema wameridhishwa na kikao cha leo na kwamba mambo ambayo wameafikiana yatatekelezewa. 

Godfriend Mbuya 

Januari 13, 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment