Responsive image
Responsive image
Posted : January 12, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein
Responsive image

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema wananchi wanapaswa kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Magufuli katika kuwaleta maendeleo Watanzania.

Dkt. Shein ameyasema hayo katika uwanja wa Amani mjini Unguja wakati wa maadhimisho ya miaka 54 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kusema kuwa Rais Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya vitendo vinavyorudisha nyuma maendeleo.

Katika hotuba yake Dkt. Shein ameeleza mafanikio makubwa ambayo serikali yake imeyapata ikiwa  ni pamoja na kuongezeka kwa watalii ambao wanasaidia kuongeza pato la serikali huku akiahidi kutoa  elimu bure kwa shule za msingi na sekondari kuanzia Julai mwaka huu..

Viongozi mbalimbali wamehudhuria sherehe hizo akiwemo Rais Dkt. John Magufuli.

Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yalifanyika tarehe 12 Januari mwaka 1964 kwa lengo la kumkomboa mwananchi kutoka kwenye utawala dhalimu wa kikoloni.

DARLING SAID

JANUARI 12, 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment