Responsive image
Responsive image
Posted : January 12, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Donald Trump wa Marekani
Responsive image

Rais Donald Trump wa Marekani anadaiwa kuwatusi wahamiaji wanaoingia nchini humo kwa kusema kuwa wanatoka katika nchi chafu, ambapo inasemekana kuwa tamko hilo liliwalenga watu kutoka Afrika, Haiti Na Elsavador.

Rais Trump ametoa kauli hiyo wakati ambapo Maseneta wa nchi hiyo wakiwasilisha makubaliano waliyofikia kuhusu wahamiaji.

Ikulu ya marekani haijakanusha kuhusu taarifa hiyo, licha ya Maseneta wengi kutoka vyama vya Republican na Democrats kupinga kauli ya Trump na kusema kuwa ni ya kibaguzi.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment