Responsive image
Responsive image
Posted : January 12, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Maporomoko ya ardhi katika jimbo la California Marekani
Responsive image

Juhudi za kuokoa watu waliofukiwa na maporomoko ya udongo katika jimbo la California zinaendelea ambapo hadi sasa watu wanane hawajulikani walipo.

Serikali ya California imetoa orodha ya majina ya watu 17 waliopoteza maisha katika tukio hilo ambapo baadhi yao ni watoto wenye umri wa kuanzia miaka mitatu hadi 10 na wengine ni wazee wa miaka 80.

Maporomoko hayo ya udongo yaliyoambatana na mafuriko yamesababisha uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu na habari zinasema moto wa msituni uliozuka nchini humo mwezi uliopita ndio umechangia kwa kiasi kikubwa maporomoko ya udongo.

Zaidi ya nyumba 100 zimeharibiwa kabisa, huku nyingine zaidi ya 300 zikiwa zimeathiriwa na maporomoko hayo.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment