Responsive image
Responsive image
Posted : January 11, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Maandamano nchini Tunisia
Responsive image

Kumekuwa na muendelezo wa siku tatu za maandamano na ghasia nchini Tunisia katika mji mkuu wa Tunis na miji mingine ya nchi hiyo.

Polisi wamekuwa wakirusha mabomu ya machozi kwa kundi kubwa la watu ambao wamekuwa wakilalamikia juu ya mfumuko wa bei ambao unaathiri upatikanaji wa mahitaji muhimu.

Waziri mkuu , Youssef Chahed amelaani maandamano hayo akidai kuwa hayakubaliki kwa kuwepo kwa fujo za waandamanaji.

Kwa upande wao waandamanaji ,nao pia wametoa malalamiko yao dhidi ya polisi.

Kwa mujibu wa BBC wafanyabiashara wengi wamekamatwa na polisi na kuibiwa huku vyombo vya usalama wakiwa wamewekea mkazo kulinda majengo ya serikali.

Watu wapatao 200 wamefungwa mpaka sasa huku kukiwa na mpango mwingine wa kuwepo kwa maandamano mengine makubwa hapo kesho.

Chanzo BBC

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment