Responsive image
Responsive image
Posted : January 10, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Agustino Mrema
Responsive image

Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Augustino Mrema amesema kuwa taarifa za kifo alizozushiwa hivi karibuni zimesababisha athari kubwa kwake pamoja na familia yake na hivyo ameanza kufuata utaratibu wa 'kuwashughulikia' waliotangaza uzushi huo.

 

Akizungumza katika mahojiano maalum na TBC, Mrema ambaye aliambatana na mke wake amewataka watanzania kutumia vyema mitandao ya kijamii kwa manufaa yao kiuchumi na kijamii na kuepuka kuzusha habari zisizokuwa na ukweli .

“Taarifa zilizosambazwa zimeleta mtafaruku kwa familia yangu kwa rafiki zangu na jamii kwa ujumla, mimi hawa lazima niwafundishe adabu, nimetoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA na wameniuliza ninataka shilingi ngapi, nikawaambia ninadai bilioni 20”, amesema Mrema.

Sambamba na hayo Mrema ameongeza kuwa mitandao ya kijamii isipotumia vizuri inaweza kuleta athari kubwa katika jamii na kuathiri shughuli za maendeleo.

Naye mkewe Bi Rose Mrema, amesema ni vyema mitandao ya kijamii ikatumika ipasavyo ili kuepusha taharuki inayoweza kujitokeza kwa kuitumia vibaya.

GODFRIEND MBUYA

JANUARI 10, 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment