Responsive image
Responsive image
Posted : January 10, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Moto mkubwa uliosababishwa na mafundi wa DAWASCO Dar es salaam
Responsive image

Mkurugenzi mkuu wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeje amesema watafanya tathmini ya hasara iliyosababishwa na moto huko Buguruni Dar es salaam na kulipa fidia.

Moto mkubwa umezuka katika eneo la Buguruni wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam na kusababisha nyumba moja na nguzo mbili za umeme kuteketea wakati wafanyakazi wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASCO) wakiweka mabomba mapya ya maji na kupasua bomba la gesi la SONGAS.

Naye Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto wilaya ya Ilala Mrakibu msaidizi Uli Mburuko, amesema moto huo umesababisha uharibifu wa mali mbalimbali ikiwemo nyumba  na nguzo za umeme.

BAKARI MWARABU

10 JANUARI 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment