Responsive image
Responsive image
Posted : January 10, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Maporomoko ya ardhi katika jimbo la California Marekani
Responsive image

Watu 13 wamekufa kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa kusini mwa jimbo la California nchini Marekani.

Watu wengine 163 wamelazwa hospitali wakipatiwa matibabu, huku watu wapatao 300 wanadaiwa kukwama, mashariki mwa mji wa Santa Barbara.

Mafuriko na maporomoko ya ardhi yameathiri baadhi ya maeneo ambayo yaliathiriwa na moto mkubwa wa nyika na yameharibu barabara kuu ya pwani umbali wa maili 30.

Maafisa wa uokoaji wamesema kuna watu kadha ambao hawajulikani waliko na kwamba idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka.

BBC SWAHILI

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment