Responsive image
Responsive image
Posted : January 09, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John Magufuli na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa
Responsive image

Rais Dkt. John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Katika mazungumzo hayo Lowassa amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya na ametaja baadhi ya maeneo ambayo kazi kubwa imefanyika kuwa ni kutoa elimu bila malipo, ujenzi wa mradi wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge), ujenzi wa viwanda na ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) ambavyo vinazalisha ajira nyingi kwa Watanzania.

Kwa upande wake Rais Magufuli amempongeza Lowassa kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na serikali na kusema Lowassa ni mmoja wa viongozi ambaye kwa wakati wake ametoa mchango mkubwa katika nchi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Lowassa kukutana na Rais Ikulu tangu Rais Magufuli aingie madarakani.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment