Responsive image
Responsive image
Posted : January 09, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Baadhi ya wanajeshi wa Tanzania wanaolinda amani chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa
Responsive image

Wanajeshi kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaolinda amani chini ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika (UNAMID) katika jimbo la Darfur, Sudan Kusini wametakiwa kujiandaa kujiunga na  kikundi maalum kitakachofanya kazi katika safu za milima ya Jaber maeneo ambayo hayakufikiwa na Umoja wa Mataifa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi wa amani Sudan, Luteni Jenerali Leonard Ngondi ambaye amefanya ziara katika kambi za Khorabeche na Minawashe ambako kuna askari wa kulinda amani kutoka nchini Tanzania.

Amesema kinachosubiriwa sasa ni tamko la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa  ili kutoa mwelekeo wa  utekelezaji wa awamu ya pili ya upunguzaji idadi ya vikosi vya walinda amani baada ya awamu ya kwanza kukamilika

Ameongeza kuwa ana imani na wanajeshi kutoka Tanzania na kwamba hakuna shaka kazi yao itafanyika kwa weledi mkubwa.

Hivi karibuni Tanzania chini ya mwamvuli wa UNAMID kupitia kikosi cha Tanzbatt 11 kinachoongozwa na kanali William Sandy kilifanikiwa kufika katika maeneo ya Jaber ambayo yalikuwa hayafikiki kutokana na miundombinu mibovu na kukaliwa na waasi.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment