Responsive image
Responsive image
Posted : January 09, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa
Responsive image

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amewataka wakulima wa zao la korosho mkoani humo  kubadili miche ya zamani ya korosho na kupanda miche ya kisasa ili kuongeza uzalishaji zaidi wa zao hilo.

Byakanwa amesema kukua na kuimarika kwa bei ya korosho nchini kumesababisha mikoa mingine kuanza kulima zao hilo hivyo wakulima wa Mtwara wanapaswa kuongeza uzalishaji ili kuendelea kuwa mkoa unaoongoza kwa uzalishaji wa zao hilo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Nchini Hassan Jarufu amesema wamedhamiria kufufua viwanda vya ubanguaji wa korosho ghafi  ili kulinda soko la ndani.

Kufuatia juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha  bei ya zao la korosho inakuwa na kuimarika wananchi kutoka mikoa mbalimbali wanachangamkia fursa ya kulima  zao hilo.

 

MARTINA NGULUMBI

JANUARI 09, 2017

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment