Responsive image
Responsive image
Posted : January 09, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Kocha wa Real Madrid Mfaransa Zinedine Zidane
Responsive image

Kocha wa Real Madrid Mfaransa Zinedine Zidane amesema mafanikio yake kipindi alipokuwa mchezaji wa timu hiyo hayawezi yakamsaidia kuokoa kibarua chake cha ukocha ambacho kipo shakani kwa sasa.

Zidane aliyeiongoza Real Madrid kutwaa mataji mawili ya ligi ya mabingwa barani Ulaya pamoja na ubingwa wa ligi kuu ya Hispania Laliga, kwa sasa anakabiliana  na shinikizo kubwa ndani ya timu hiyo kutokana na kufanya vibaya kwenye Laliga msimu huu.

Madrid ipo katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Laliga, ikiwa imeambulia ushindi katika michezo 9 kati ya 19 iliyocheza msimu huu na ipo alama 16 pungufu dhidi ya kinara wa ligi hiyo timu ya Barcelona jambo linalomuweka kwenye wakati mgumu kocha huyo.

Akizungumzia hali ilivyo hivi sasa kwenye kikosi chake, kocha Zidane amesema hajioni akiendelea kuwa kocha wa timu hiyo kwa miaka 10 ijayo kwani makocha hawadumu kwenye timu, tofauti na wachezaji ambao hata kama hawatafanya vizuri kwa msimu mmoja wanaweza kuvumiliwa na kusalia kwenye timu.

Zinedine Zidane amekuwa kocha wa Real Madrid tangu Januari 2016 aliporithi mikoba ya kocha Carlo Ancelloti

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment