Responsive image
Responsive image
Posted : January 08, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Profesa Shukrani Manya akiapishwa kuwa Kamishna wa Madini
Responsive image

Rais Dkt. John Magufuli amemteua Prof. Shukrani Manya kuwa kamishna wa Madini

Rais Magufuli ametangaza uteuzi huo  leo Ikulu jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kumuapisha Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko aliyeteuliwa aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika hafla hiyo Magufuli amesema haridhishwi na utendaji kazi wa baadhi ya viongozi aliowateua kwani umekua wa kusua sua hali inayochelewesha maendeleo kwa wananchi wanaowatumikia.

Rais Dkt. John Magufuli amesema utendaji usioridhisha wa baadhi ya viongozi katika Wizara ya Madini umepelekea kutosainiwa kwa kanuni za sheria namba saba ya Madini ya mwaka 2017 na akatoa agizo kwa Waziri wa Katiba na Sheria Palamagamba Kabudi kuhakikisha kanuni hizo zinasainiwa kabla ya ijumaa ya tarehe 12 mwezi huu.

Rais Magufuli ameongeza idadi ya Manaibu Waziri katika Wizara ya Madini kutokana na Wizara hiyo kuwa na mambo mengi yanayohitaji nguvu kazi ya kutosha.

MARY MNDEME

08 JANUARI 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment