Responsive image
Responsive image
Posted : January 08, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Responsive image

Mtaji mkubwa wa soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) umeongezeka kwa asilimia 10.11% kwa mwaka 2017 ikilinganisha na mwaka 2016 na mtaji wa soko wa makampuni ya ndani pia umeongezeka kwa asilimia 31.05% kwa mwaka 2017.

Taarifa ya DSE imeonyesha kuwa ndani ya Mwaka 2017 pia kulikuwa na mauzo ya awali ya hisa za Vodacom Tanzania Plc ambayo yamechangia ongezeko la wawekezaji 40,000 na pia kukuza mtaji wa soko kwa takribani trilioni 2.

Mauzo ya hisa kwa mwaka 2017 yameongezeka kutoka Shilingi bilioni 420 ya mwaka 2016 hadi Shilingi bilioni 510 ya mwaka 2017 na idadi ya hisa zilizouzika na kununiliwa sokoni pia imeongezeka kutoka hisa milioni 194 mwaka 2016 hadi hisa milioni 257 kwa mwaka wa 2017.

Kwa upande wa hatifungani, mwaka 2017 hati fungani zenye thamani ya Shilingi bilioni 748.7 ziliuzwa kwa gharama ya shilingi bilioni 653 Hilo ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na mwaka 2016 ambapo hati fungani zenye thamani ya shilingi bilioni 556.7 ziliuzwa kwa gharama ya shiliningi bilioni 428.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment