Responsive image
Responsive image
Posted : January 07, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua mradi wa kupoozea umeme, Unangwa, Songea mkoani Ruvuma
Responsive image

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka jamii kulinda miundombinu ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) wakati wa ujenzi wa miradi mbalimbali ya umeme.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha kupozea umeme kilichopo Unangwa Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema kukamilika kwa mradi wa umeme wa Makambako Songea utafungua fursa za uwekezaji Mkoani Ruvuma kwa kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika.

Waziri Mkuu Majaliwa pia ameweka jiwe la msingi katika Kituo cha Kupozea Umeme cha Unangwa na Ofisi ya TANESCO Mkoa wa Ruvuma.

NOELA NJAWA

07 JANUARI 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment