Responsive image
Responsive image
Posted : January 07, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) Jaji Semistocles Kaijage
Responsive image

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) Jaji Semistocles Kaijage amesema kanuni na sheria za uchaguzi zilizopo zinajitosheleza kutatua changamoto zinazojitokeza katika chaguzi ndogo.

Akizungumza katika mkutano wa NEC na viongozi wa vyama vya siasa juu ya maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Majimbo matatu na Kata sita unaotarajiwa kufanyika Tarehe 13 mwezi huu Jaji Kaijage amesema tatizo lililopo ni wanasiasa kutofuata utaratibu wa kisheria katika kutatua changamoto hizo.

Mkutano huo uliandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa  viongozi wa vyama vya siasa kwa lengo la kutoa taarifa ya maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Longido, Singida Kaskazini  na Songea Mjini pamoja na Kata sita zilizoko katika mikoa mbalimbali.

Pamoja na uchaguzi mdogo wa Majimbo matatu na Kata sita utakaofanyika Tarehe 13 mwezi huu pia Tume ya Uchaguzi imeanza maandalizi ya uchaguzi mwingine mdogo unaotarajiwa kufanyika Tarehe 17 mwezi ujao katika Majimbo ya Kinondoni na Siha pamoja na Kata nne. 

MARY MNDEME

07 JANUARI 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment