Responsive image
Responsive image
Posted : January 07, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Samaki aina ya Sangara
Responsive image

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ameagiza kupigwa mnada kwa zaidi ya tani sitini na tano za samaki waliokaushwa aina ya Sangara ambao walikamatwa hivi karibuni  katika kisiwa cha Rubili wilayani Muleba Mkoani Kagera.

Samaki hao wakamatwa wakiwa wamehifadhiwa katika magunia tayari kusafirishwa kinyume na sheria ya uvuvi namba 22 ya mwaka 2003,huku mmiliki wake akitokomea kusikojulikana.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amewasili Mkoani Kagera na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu ambaye amezungumzia changamoto inayoikabili sekta ya uvuvi katika udhibiti wa uvuvi haramu.

Kisha Waziri Mpina akatembelea kituo cha uvuvi kanda ya Kagera ambapo zaidi ya tani 65 za samaki aina ya sangara waliokaushwa wamehifadhiwa. Waziri Mpina ameagiza shehena hiyo ya samaki kupigwa mnada mara moja kwa kufuata taratibu zote za kisheria.

Aidha Waziri Mpina ameagiza Maafisa wa idara za uvuvi nchini kutotoa leseni mpya kwa wasafirishaji wa mazao ya uvuvi hadi pale watakapowasilisha nyaraka za malipo ya kodi kutoka TRA.

 

CHARLES MWEBEYA

07 JANUARI 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment