Responsive image
Responsive image
Posted : January 07, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Kocha aliyetimuliwa Stock City Mark Hughes
Responsive image

Baada ya kipigo kutoka timu ya daraja la pili ya Coventry City kwenye mchezo wa kombe la FA, timu ya Stoke City imemfuta kazi aliyekuwa kocha wake - Mark Hughes kutokana na mfululizo wa vipigo kwenye michezo mitano iliyopita.

Timu hiyo imeambulia vipigo vitano kwenye michezo saba ya ligi kuu ya England na kuifanya iteremke mpaka kwenye eneo la hatari la kushuka daraja na kumfanya kocha Hughes kuwa kwenye wakati mgumu kwenye kikosi hicho.

Katika mchezo dhidi ya Coventry ambao Stoke City wamelazwa kwa kufungwa mabao mawili kwa moja, baadhiya mashabiki wa timu hiyo walibeba mabango yanayoshinikiza kufukuzwa kazi kocha Hughes.

Kwa upande wake kocha huyo ambaye amekiongoza kikosi cha timu hiyo kwenye michezo 200 amesema alikuwa anatambua kuwa matokeo ya mchezo dhidi ya Coventry yasingebadili msimamo wa uongozi wa kumtimua kazi kwani hatima yake ndani ya timu hiyo ilikuwa shakani kwa muda mrefu.

Kabla ya kuwa kocha wa Stoke City, Hughes amewahi kuvinoa vilabu vya Manchester City, Blackburn Rovers, Fulham na Queens Park Rangers.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment