Responsive image
Responsive image
Posted : January 06, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John Magufuli
Responsive image

Rais Dkt. John Magufuli amemteua  Mbunge wa jimbo la Bukombe Doto Biteko aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya muda iliyochunguza dhuluma dhidi ya mapato ya nchi katika biashara ya madini ya Tanzanite, kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Gerson Msigwa, Rais Magufuli amefanya uteuzi huu kwa lengo la kuongeza nguvu kutokana na wingi wa majukumu katika Wizara hiyo.

Biteko anatarajiwa kuapishwa Jumatatu Januari 8, Ikulu jijini Dar es salaam.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amekwenda kumjulia hali Mzee Kingunge Ngombale  Mwiru aliyelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili akipatiwa matibabu .

Mzee Kingunge amelazwa hospitalini hapo akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake jijini Dar es salaam. 

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment