Responsive image
Responsive image
Posted : January 06, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Hali ya baridi kali iliyoambatana na kuanguka kwa theluji
Responsive image

Watu kumi na tisa wameripotiwa kufa tangu kuanza kwa msimu wa baridi kali na kuanguka kwa theluji katika maeneo mbalimbali ya mashariki mwa Marekani.

Taarifa kutoka nchini humo zinaarifu kuwa bado kumekuwa na hali ya baridi kali na theluji katika maeneo ya makazi na yale ya huduma za kijamii ambapo baadhi ya watu wameondolewa katika makaazi yao ili kuepuka maafa zaidi yanayoweza kujitokeza.

Idara ya Taifa ya Utabiri wa hali ya Hewa nchini Marekani (NWS) imetahadharisha kwamba hali ya  baridi na kuanguka kwa theluji  itaendelea kuwa mbaya mashariki mwa Marekani.

Usafiri wa umma na safari za mashirika mbalimbali ya ndege umeathiriwa kutokana na hali hiyo huku juhudi mbalimbali za kuuondoa theluji katika miundombinu ya barabara na viwanja vyandege zikiendelea kufanyika.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment