Responsive image
Responsive image
Posted : January 05, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Kitabu cha Fire and Fury kinachoibua kashfa dhidi ya Rais wa Marekani Donald Trump
Responsive image

NI 'Fire and Fury' au kwa Kiswahili inaweza kutafsirwa 'Moto na Hasira'. Hiki ni kitabu kipya kabisa kilichoandikwa na Mmarekani Michael Wolff ambaye anadai amefanya utafiti kwa kuhoji zaidi ya watu 200 na kugundua kuwa hata sehemu kubwa ya wafanyakazi wa Ikulu ya Marekani wanamuelezea Rais Donald Trump kuwa ni sawa na mtoto kwa vile anachohitaji yeye ni kusifiwa tu kwa haraka.

" Ni mtu anayehitaji kusifiwa mara moja kwa yale anayoyafanya. Yote ni kuhusu yeye tu na sio kingine. Huyu mtu ambaye hasomi chochote ili kujifunza na hataki kusikiliza chochote. Ni mtu aliye tayari kumsukumia mbali yeyote yule anayetofautiana naye" amesema   Wolff kwenye kitabu chake.

Hayo yametokea wakati Rais Trump akidai kuwa kitabu hicho kimejaa uongo na kwamba yeye hajawahi hata kuzungumza na mwandishi huyo, ingawa Wolf ameiambia televisheni ya NBC kwamba alifanikiwa kupata saa tatu za kuzungumza na Trump.

Kwa kutumia wanasheria Rais Trump amekuwa akifanya jitihada kubwa za kuzuia kitabu hicho kisizinduliwe wala kuuzwa, lakini kutokana na uimara wa mfumo wa Demokrasia huko Marekani ameshindwa kufanya hivyo.

Kitabu cha 'Fire and Fury' kimeanza kuuzwa leo hii nchini Marekani ambapo imedaiwa kuwa watu wengi wamejitokeza kukinunua.

Katika ukurasa wake wa "Twitter' jana Ijumaa, Rais Trump amesema kitabu hicho alichokiita kuwa ni cha kizushi kimekuwa kinashinikizwa na waandishi wa habari na watu wengine wenye nia ovu dhidi yake. 

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment