Responsive image
Responsive image
Posted : January 04, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt John Magufuli akipokea barua ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda iliyowasilishwa kwake na Mjumbe Maalum Sam Kutesa.
Responsive image

Rais Dkt John Magufuli amepokea barua kutoka kwa Rais Yoweri Museveni wa Uganda iliyowasilishwa na Mjumbe Maalum Sam Kutesa ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Jijini Dar es salaam imesema pamoja na kupokea barua hiyo Rais Magufuli amefanya mazungumzo na Kutesa Ikulu Jijini Dar es salaam .

Baada ya mazungumzo hayo Mjumbe huyo Maalum wa Rais Museveni amemtumia Rais Magufuli na Watanzania wote salamu za heri ya mwaka mpya na pia wamezungumzia masuala yanayohusu uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda.

Amesema Uganda inafurahishwa na uhusiano mzuri wa kidugu uliopo kati yake na Tanzania na kwamba mazungumzo ya leo yalijikita kuuimarisha zaidi uhusiano huo kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment