Responsive image
Responsive image
Posted : January 04, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John Magufuli akisalimiana na Profesa Beno Ndulu
Responsive image

Rais Dkt. John Magufuli, ameagana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania  (BoT)  anayemaliza muda wake Prof. Benno Ndulu Ikulu Jijini Dar es salaam.

Baada ya mazungumzo yao, Prof. Ndulu amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumuamini na kufanya nae kazi tangu alipoingia madarakani na amesema kuwa anafurahi kumaliza kipindi chake huku uchumi wa nchi ukiwa mzuri. Prof. Ndulu amempongeza Rais Magufuli kwa miongozo muhimu iliyosaidia kuimarisha uchumi ikiwemo kudhibiti mfumuko wa bei.

 Kwa upande wake Rais Magufuli amempongeza Prof. Ndulu kwa utumishi wake wa miaka 10 na kazi nzuri aliyoifanya kusimamia uchumi.

Rais Dkt. Magufuli pia amezungumza na Gavana Mteule Prof. Florens Luoga ambaye amemshukuru Rais Magufuli kwa uteuzi huo na kusema taarifa zinazotolewa na BoT kuhusu ukuaji wa uchumi zinaandaliwa kitaalamu na kwa kushirikisha vyombo mbalimbali vikiwemo Benki ya Dunia.

Wakati huo huo, Rais Dkt. Magufuli amesema mwezi ujao Serikali itatoa Shilingi Bilioni 200 kulipa madeni ya ndani yatakayokuwa yamehakikiwa yakiwemo ya wazabuni mbalimbali waliotoa huduma katika taasisi za Serikali, madai ya watumishi wa serikali kama vile walimu na madai ya wakandarasi wa ndani.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment