Responsive image
Responsive image
Posted : January 04, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmod Hamid
Responsive image

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema uchaguzi mdogo katika Majimbo ya Siha Mkoani Kilimanjaro na Kinondoni Mkoani  Dar es salaam  pamoja  na  Kata nne  za Tanzania Bara utafanyika Tarehe 17 mwezi ujao.

Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmod Hamid amesema uchaguzi huo utafanyika kufutia wabunge hao kujivua uanachama wa vyama vyao na kukosa sifa za kuendelea kuwa wabunge.

Jaji Mstaafu Hamid amesema fomu  za  uteuzi  kwa  majimbo  hayo  mawili  na  kata  nne  itakuwa  kati ya tarehe  14 na 20 mwezi huu na uteuzi  wa  wagombea  utafanyika  tarehe  20 na kampeni zitaanza tarehe  21 Januari hadi Tarehe 16 Februari. Pia amevikumbusha vyama vya Siasa na wadau wote wa uchaguzi  kuzingatia sheria kanuni taratibu miongozo na maelekezo yote wakati  wa uchaguzi huo mdogo.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment