Responsive image
Responsive image
Posted : January 04, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Responsive image

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuna haja ya kuangalia namna ya kubadili mfumo uliopo hivi sasa wa kucheza mechi kila baada ya siku hasa kwenye msimu wa sikukuu kwani unaweza kupelekea kupoteza maisha kwa wachezaji.

Guardiola ameyasema hayo kutokana na wachezaji wake muhimu kupata majeraha ambayo kocha huyo anaona yanasababishwa na msongamo wa mechi katika kipindi hiki ambacho ligi nyingine zimesimama kupisha mapumziko ya msimu wa sikukuu.

Timu hiyo imempoteza mshambuliaji wake Gabriel Jesus aliyeumia kwenye mechi dhidi ya Crystal Palace pamoja na Kevin De Bruyne ambaye pamoja na kuwa na maumivu alicheza mchezo wa jana huku Kyle Walker akisikilizia maumivu aliyoyapata kwenye mchezo wa jana dhidi ya Watford.

Katika matokeo ya mchezo huo, vinara hao wa ligi hiyo Manchester City wamerejesha makali yao ya ushindi baada ya kuibabua Watford mabao matatu kwa moja na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Mapema katika dakika ya kwanza Raheem Sterling aliiandikia Manchester City bao la kuongoza kabla beki Christian Kabasele wa Watford hajajifunga katika dakika ya 13 huku Sergio Aguero akiifungia Man City bao la tatu katika dakika ya 63 huku Andre Gray akifungia Watford bao pekee katika dakika ya 82.

Matajiri hao wa jiji la Manchester wamefikisha alama 62 alama 15 zaidi ya Manchester United iliyopo kwenye nafasi pili ikiwa na alama 47 baada ya kushuka dimbani mara 22.

ASHERI THOMAS

03 JANUARI 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment