Responsive image
Responsive image
Posted : January 02, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Nguza viking (Babu Seya) na mwanae
Responsive image

Rais Dkt. John magufuli amekutana na mwanamuziki Nguza Viking na watoto wake waliokwenda Ikulu jijini Dar es salaam kwa lengo la kumshukuru kwa msamaha uliopelekea kuachiwa huru yeye pamoja na mwanaye Papii Nguza waliokuwa wakitumikia kifungo cha maisha jela.

Nguza Viking akiwa na Wanawe wamezungumza na Rais Magufuli ambapo wamemshukuru kwa msamaha alioutoa kwao na kwa wafungwa wengine 61 waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo.

Kwa upande wake Rais Dkt. Magufuli amewashukuru wanafamilia hao kwa moyo wao wa shukrani kwake.

Nguza na wanawe wamemuombea Rais Dkt. Magufuli na pia kuiombea nchi na kisha mwanamuziki Papii kocha akatoa kibwagizo cha wimbo wa Seya.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment