Responsive image
Responsive image
Posted : January 02, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda
Responsive image

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), imevitoza faini ya shilingi milioni sitini kwa pamoja vituo vitano vya televisheni kwa kutangaza habari zinazokiuka kanuni za huduma za utangazaji za mwaka 2015.

Uamuzi huo umetangazwa jijini Dar es salaam na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda. 

Mapunda amesema makosa hayo yalitendeka kupitia taarifa za habari za vituo hivyo tarehe 30 Novemba 2017 na kusema kuwa vyombo hivyo vilikiuka misingi ya maadili ya uandishi wa habari.

Vyombo vya habari vilivyopigwa faini ni AZAM TWO, ITV, EATV, Channel Ten na  STAR TV.

Vituo vya Channel ten, EATV na ITV vimetozwa faini ya shilingi milioni 15 kila kimoja huku Star TV na AZAM Two vikitozwa kiasi cha shilingi milioni saba na laki tano kila kimoja.

Sambamba na faini hizo vituo vyote vimewekwa chini uangalizi wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA, kwa muda wa miezi sita kuanzia Januari pili mwaka huu.

 

ANNA MWASYOKE

02 JANUARI 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment