Responsive image
Responsive image
Posted : January 02, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine
Responsive image

Mzunguko wa 12 wa Ligi kuu soka Tanzania Bara unahitimishwa rasmi hii leo kwa kuchezwa mchezo mmoja ambapo wenyeji Mbeya City wanawakaribisha  Kagera Sugar katika dimba la kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mchezo huo ulikuwa uchezwe jana lakini ukalazimika kuahirishwa baaada ya mvua kubwa kunyesha mkoani humo na kuuacha uwanja katika hali ambayo mchezo usingeweza kufanyika.

Katika mchezo mmoja uliochezwa hapo jana kwenye dimba la Mwadui Complex wenyeji wa uwanja huo, timu ya Mwadui imeisasambua timu ya Ruvu Shooting kwa mabao mawili kwa moja.

Mabao yote ya Mwadui Fc yamepachikwa kimiani na mshambuliaji Paul Nonga huku bao la kufutia machozi la Maafande wa Ruvu Shooting likipachikwa na Adam Ibrahim.

Mara baada ya mchezo wa leo kati ya Mbeya City na Kagera Sugar ligi itasimama kwa muda kupisha michuano ya kombe la Mapinduzi ambalo linaendelea kutimua vumbi huko visiwani Zanzibar.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment