Responsive image
Responsive image
Posted : January 01, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Rais John Magufuli
Responsive image

Rais John Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kufuatia ajali ya barabarani iliyosababisha vifo vya watu 36 baada ya basi la abiria kugongana na lori katika barabara ya Nakuru - Eldoret nchini Kenya.

Katika salamu hizo Rais Magufuli amesema msiba huo umesababisha majonzi makubwa sio tu kwa Wakenya bali pia kwa wana Jumuiya ya Afrika Mashariki wote.

Rais Magufuli amesema kwa niaba ya Watanzania wote anampa pole Rais Kenyatta na wana familia wote waliowapoteza jamaa zao na pia wananchi wote wa Kenya. Amesema anaungana nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na kuwaombea majeruhi wote wa ajali hiyo wapone haraka na marehemu wote wapumzishwe mahali pema.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment