Responsive image
Responsive image
Posted : January 01, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda
Responsive image

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda ameahidi kubeba gharama za uendeshaji za uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam zinazohusu mkesha wa mwaka mpya kuanzia mwaka huu wa 2018.

Makonda ametoa ahadi hiyo wakati wa mkesha wa kuuaga mwaka 2017 na kuliombea taifa uliofanyika usiku wa kuamkia leo, katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam ambapo pia ameiomba wizara ya habari, utamaduni sanaa na michezo kuondoa gharama kwa waandaaji wa mkesha wa kuliombea Taifa unaofanyika kila mwaka Disemba 31.

Katika hatua nyingine Makonda amewataka watanzania kuwaombea viongozi wa serikali akiwemo Rais Dkt John Magufuli ili waendelee kutenda vyema katika majukumu yao.

Makonda amesema atendelea kuimarisha amani katika mkoa wake huku akiwataka watanzania kutunza tunu hiyo kwa kuwa ndio sifa kubwa ya taifa na kwamba pasipo amani hakuna maendeleo.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment