Responsive image
Responsive image
Posted : December 31, 2017 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba
Responsive image

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba amesema shirika hilo litaendelea kusimamia haki maadili na utamaduni katika utoaji wa habari kwa watanzania  bila kujali itikadi zao.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum na TBC katika Kipindi cha Jambo Tanzania Dkt. Rioba amesema katika kufanikisha hilo tayari TBC inaendelea kuboresha usikivu wa matangazo yake hususan katika maeneo ya pembezoni.

Pia amesema Shirika la Utangazaji Tanzania litaendelea kuboresha maudhui yake ili  kuwavutia vijana waweze kujifunza kutoka TBC na  kuendeleza falsafa ya ukombozi.

Katika hatua nyingine Dkt. Rioba amesema TBC imejipanga mwanzoni mwa mwaka 2018 kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kuhamia Dodoma ambapo tayari  imeanza maandalizi ya awali ya ujenzi wa jengo kubwa  la TBC.

Amesema pia kuwa TBC ndio shirika pekee lenye wafanyakazi walio na elimu ya juu kuliko shirika lolote hapa nchini na litaendelea kuwahudumia wananchi kwa kutoa habari bora na kuandaa vipindi vyenye kuleta tija kwa wananchi.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment