Responsive image
Responsive image
Posted : December 31, 2017 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora George Mkuchika
Responsive image

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora George Mkuchika amezitaka halmashauri zote za kanda ya kusini kuhakikisha zinapeleka wanafunzi katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Mtwara ili waweze kujiendeleza.

Waziri Mkuchika ameyasema hayo alipofanya ziara ya kutembelea chuo hicho kwa ajili ya kukagua miundombinu yake kuona namna kinavyofanya kazi, mafanikio pamoja na changamoto zake.

Pamoja na kuwepo kwa changamoto kadhaa waziri Mkuchika ameridhika kuwa chuo hicho kinaweza kusaidia kupata wataalamu wataoweza kusaidia mikoa ya kusini na hivyo akaziagiza halmashauri kuwa mbele katika kutumia fursa ya kuwepo kwa chuo hicho mkoani Mtwara.

Akisoma taarifa ya chuo kwa Waziri huyo mkuu wa chuo Emmanuel Timbika amesema pamoja na mafanikio lakini bado chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mabweni.

MARTINA NGULUMBI

DISEMBA 31, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment